May 2015


AY ana stock ya muziki mpya inayoweza kutengeneza zaidi ya album nne.
Akiongea kwenye kipindi cha Mlimanidotcom cha Mlimani TV, rapper huyo amesema hadi sasa ana nyimbo mpya zifikazo 90.

“Ukitaka kuhakikisha utahakikisha wewe mwenyewe binafsi lakini kwasababu siwezi kuhakikisha kwa kuweka title za nyimbo zangu lakini nina nyimbo 90 sasa hivi, nilikuwa na 88 nimeongeza na hizo ni mpya,”alisema AY.
Hata hivyo alisema bado hajafikiria kutoa album hivi karibuni.