October 2015

Baada ya uongozi wa Million Dollar Boys (MDB)
uliokuwa ukimsimamia Young Dee kusitisha
kufanya kazi na rapper huyo, CEO wa kampuni hiyo
na studio za Authentic, Millian ametoa ofa ya video
kwa kundi la Mtu Chee ambalo Young Dee pia
amejitoa.
Kundi la Mtu Chee lililoanzishwa na rappers
Stamina, Country Boy na Young Dee, leo wameachia
single mpya bila Young Dee huku wakiwa
 wamemwongeza Young Killer kwenye single hiyo. Young Dee alikaririwa hivi karibuni akidai kuwa
uongozi wake (MDB) ulimzuia kuendelea kuwa
member wa kundi hilo. Millian amethibitisha kutohusika katika maamuzi ya
Young Dee kujiondoa Mtu Chee, kwa kujitolea
 kuwapa ofa ya video ya wimbo mmoja kundi hilo. Kupitia post ya Instagram ya Country Boy, Millian
alicomment kwa kuandika;
“Natoa offa ya kuwafanyia music video yenu moja bure wanangu. Dee farasi sana alivyosema Eti management yake imemzuia kufanya Kazi Na nyie
@countryboytz
@youngkillermsodoki
@stamina shorwebwenzi”

Country boy alijibu; “thanx bro tunapokea na tunajua umuhimu wako kaka mkubwa Asante tupo tayari”




Akizungumza na kipindi cha XXL, Mabeste alisema
 hata akiachana na mpenzi wake Lisa ataendelea
 kubaki na tattoo hiyo kama kumbukumbu kwenye
maisha yake. “Hata kama let say mfano tumeachana, nitakuja
 kuanzisha maisha mengine na mke mwingine, yeye
 ataendelea kuwepo kwenye maisha yangu,”
alisema. “Tayari tupo na mtoto na ndio ni kitu
ambacho kitatuunganisha. Kwahiyo yeye ni part ya maisha yangu. Ndio maana
 nikamchora sio kuna siku moja nitamsahau.


Mimi nimechora kwa ridhaa yangu na yeye kachora kwa
ridhaa yake na yote tumefanya kwa sababu ya
maumivu tuliyopitia kwenye maisha yangu,”
aliongeza Mabeste.



Mshindi wa tuzo za Afrimma 2015, Vanessa Mdee
amesema ni fahari kufananishwa kwa video ya
wimbo wake ‘Never Ever’ na video ya ‘Dance Like
We’re Making Love’ ya Ciara. 



Vanessa ameiambia Friday Night Live ya EATV
 kuwa msanii binafsi kama yeye kufananishwa na
kazi ya Ciara aliye chini record labels kubwa
duniani ni kitu kikubwa. “I think it’s great kusema ukweli, the thing about
this, Ciara ni msanii ambaye amefanya muziki kwa
muda mrefu sana.  Two ana support ya major labels,
mimi ni independent artist, najipanga peke yangu,
so as an independent artist somebody ana
compare kazi yangu na msanii wa kimataifa, it’s fine,” alisema Vanessa.

“Hamna idea ambayo utashoot ambayo mtu
hajafanya, watu wameshafika kila sehemu, watu
wameshashoot ndani ya maji, wakipaa angani sasa
utafanya nini? Unajua by the way nimesikia nyingi,
Ciara, Nicki Minaj,” aliongeza.





Chris Brown ameendelea kuudhihirishia
ulimwengu mapenzi ya dhati aliyonayo kwa
mwanaye wa kike Royalty mwenye umri wa
mwaka mmoja. Baada ya kuamua album yake mpya kuipa jina la
mwanaye huyo ‘Royalty’, sasa staa huyo wa R&B
 ametoa cover ya album hiyo yenye picha ya yeye
 akiwa amembeba mtoto wake anaye onekana
amesinzia.

Toka Breezy afahamu kuwa ana mtoto na
aliyewahi kuwa model Nia Guzman, amekuwa
akionesha jinsi gani anajivunia kuwa baba na kwa
 kiasi gani mtoto huyo amemuongezea furaha
kwenye maisha yake.

Album ya ‘Royalty’ imepangwa kutoka Nov.27.

Kundi maarufu la Uingereza la One Direction,
huingiza pauni 19,000 kila siku ambazo ni zaidi ya
shilingi milioni 62.

Waimbaji hao waliopata mafanikio baada ya kuwa
chini ya usimamizi wa Simon Cowell kupitia kipindi
cha The X Factor mwaka 2010, huingiza kiasi hicho
cha fedha kufuatia taarifa zao za fedha
 zilizochapishwa na Companies House.

One Direction walitengeneza faida ya jumla ya
 £35m na kampuni yao 1D Media mwaka jana
ingawa mwenzao Zayn Malik alijiondoa na
kuwaacha Harry Styles, Liam Payne, Niall Horan na
Louis Tomlinson.

Pamoja na mafanikio hayo, vijana hao wameamua
kupumzika mwakani baada ya kuachia album tano
na kufanya ziara nne.