2015






Stori za beki wa kati na nahodha wa klabu ya Mbeya City aliyewahi kutamba na SimbaJuma Nyosso amerudi katika headlines November 27, baada ya Chama cha Wachezaji Soka Tanzania (Sputanza) kuwasilisha ombi la kuomba Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kupitia upya hukumu ya Juma Nyosso.
Katibu mkuu wa Sputanza Abeid Kasabalala amethibitisha kuwasilishwa kwa ombi hiloTFF na kupitia kwa afisa mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Boniface Wamburawamethibitisha kuridhia kupitia upya hukumu ya Juma Nyosso, bali hiyo sio  rufaa ni ombi ambalo Sputanza wamewasilisha sambamba na kulipa Tsh 500,000/= ili ipitiwe upya adhabu ya Nyosso kwani ni kubwa sana kwa mchezaji



Juma Nyosso alifungiwa kucheza soka miaka miwili na kutakiwa kulipa faini ya Tsh milioni 2 baada ya kumfanyia kitendo cha kidhalilishaji nahodha wa Azam FC John Bocco September 27 katika mchezo kati ya Mbeya City dhidi ya Azam FC uliyochezwa katika dimba la Azam Complex Chamazi na Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 2-1.




Zimepita siku chache tu toka Justin Bieber atangaze kuanza kwa tour yake ‘Purpose world tour ‘ mwanzoni wa mwaka 2016, tour itakayompeleka nchi 56 kwa ajili ya kuitangaza Album yake mpya, PURPOSE.
Licha ya ticket za tour hiyo kuuzwa bei ya juu, mitandao mingi Marekani imekuwa ikiripoti kasi ya ticket hizo kununuliwa huku wengine wakisema mwaka 2015 umeishia kuwa mwaka poa sana kwa Justin Bieber… Lakini kingine kikubwa cha kujua kuhusu tour hii nipackage special ya VIP Selfie itakayopatikana kwenye tour ya Justin itakayoanza mwezi March mwaka 2016!

Kwa mujibu wa Altitude Tickets, package special ya VIP Selfie yani  ‘I’ll Show You VIP #Purpose Experience’ itauzwa kwa USD $925 ambayo ni sawa na milion 1,850,000, na mtu atakaponunua package hiyo itamaanisha kuwa ataweza tu kupiga picha moja ya pamoja (Group Selfie) na Justin Bieber na kushare na watu kwenye Instagram… cha kushangaza zaidi ni kwamba package hii ya ticket zimeshakwisha tayari, yani SOLD OUT!!

Package nyingine zitakazopatikana kwenye tour ya Justin Bieber ni pamoja na ‘Where Are You Now’ VIP #Purpose Experience’ kwa $325 ambayo inagonga zaidi ya 600,000za kitanzania, na ‘Ultimate #Purpose Experience’ kwa $2,000 ambayo kwa pesa ya nyumbani tunazungumzia mshiko wa milion 4 za Kitanzania!

Muimbaji wa ‘Duro’ Tekno ameingia studio na Mshindi wa Tuzo tatu za AFRIMA, Diamond Platnumz kurekodi wimbo mpya ambao utatoka wiki ijayo.


Kupitia Post aliyoiweka Instagram, Diamond ameandika
“Forget About DURO… we are about to Bang! on this New jam from my Since day one Hommie@teknoofficial …… Drops Next Week!!!! Let’s Support him #Lagos
Diamond yupo Nigeria kwa ajili ya Tuzo za Afrima ambazo tayari zimeshafanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.



Wakati akiwa Columbus kwa ajili ya show mwezi uliopita , Rapper kutoka Compton Kendrick Lamar aliwasuprise watu walioudhulia harusi hiyo bila taarifa (crush the wedding).
Kendrick akiwa na washikaji zake walivamia harusi hiyo na kuanza kucheza wimbo ambao ulikua unapiwa ukumbini hapo wa Whitney Houston “I Wanna Dance with Somebody”, mtu mmoja aliwashitukia kuwa walikua hawajaalikwa kwahiyo ikabidi awaulize kama wanafahamu wanaofunga ndoa, baada ya kushindwa kujibu, huyo mtu alibidi awafukuze, anasikika akiwaambia watoke “get the f**k out.”
Kwa mujibu wa TMZ kuna mtu mwingine alikuwa anamfahamu kendrick lamar kwa hiyo vitu vikaenda sawa. Tazama video hapo juu




Tunaposema muziki wa Tanzania unazidi kukua kimataifa, pamoja na jitihada za wasanii wenyewe, watayarishaji wa muziki wana mchango mkubwa zaidi katika mafanikio hayo.
Kwa mujibu wa Mtandao wa Bongo5 hii orodha ya watayarishaji wa muziki waliotengeneza hits nyingi zaidi mwaka 2015.
1.Nahreel (The Industry)

1. Nana – Diamond Platnumz
2. Nobody But Me – Vanessa Mdee

3. Never Ever – Vanessa Mdee
4. Nusu Nusu – Joh Makini
5. Don’t Bother –Joh Makini f/ AKA
6. Jux f/ Joh Makini – Looking For You
7. Game – Navy Kenzo
8. Visa – Navy Kenzo
9. Shem Lake – Izzo B f/ Mwana FA &G-Nako
10. Zigo – AY
11. Laini – Nick wa Pili f/ G-Nako
12. Safari – Nick wa Pili f/ Vanessa Mdee, Jux, G-Nako, Aika
13. Baba Swalehe – Nick wa Pili




2. Aby Dady (Chaiderz Records) 
20151117001826 (1)
Nyimbo alizotayarisha mwaka huu
1. Chekecha Cheketua – Alikiba
2. Nagharamia – Christian Bella f/ Alikiba
3. Subira – Cassim Mganga f/ Christian Bella
4. Nitazoea – Mo Music
5. Mule Mule – Matonya f/ Rich Mavoko
6. Zogo – Malaika
7. Ayayaa – Abdul Kiba f/ Ruby
8. Baikoko – Shebby Love f/ Beka Title
9. Mkungu wa Ndizi – Q-Chief & TID

3. Mr T-Touch (Free Nation Sound)
Touch
Nyimbo alizotayarisha mwaka huu
1. Mapenzi au Pesa – Nay wa Mitego & Diamond
2. Haye – Darassa f/ Mr Blue
3. Sina Muda – Nay wa Mitego
4. Tunaishi – Darassa f/ Nay wa Mitego
5. Nitulize – Dayna f/ Nay wa Mitego
6. Kikomo – Fred Swag f/ Barakah Da Prince
7. Nafunga Zipu –Soggy Doggy f/Baghdad & G-Nako
8. Ligi Ndogo – Billnass f/TID

4. Man Walter (Combination Sound)
Walter
Nyimbo alizotayarisha mwaka huu
1. Wanjera – Ommy Dimpoz
2. Nice Couple – Mayunga
3. Nashindwa – Christian Bella

5. Tudd Thomas (Surround Sound)
Thomas
Nyimbo alizotayarisha mwaka huu
1. Na Yule – Ruby
2. Nasema Nawe – Diamond

6. Mswaki (Black Curtains)
Mswaki
Nyimbo alizotayarisha mwaka huu
1. Sophia – Ben Pol
2. Ningefanyaje – Ben Pol
3. Watu – Heri Muziki

7. Mesen Selekta (De Fatality Music)
Mesen
Nyimbo alizotayarisha mwaka huu
1. Cheza Kwa Madoido – Yamoto Band
2. Malaika – Sare
3. Mabele – Himself
4. Cow Obama – Young Dee
5. Popo Lipopo – Pam D f/ Mesen
6. Hawashi – Snura f/ Nay wa Mitego

8. Marco Chali (MJ Records)
Marco
Nyimbo alizotayarisha mwaka huu
1. Kazi Kwanza – B.O.B Micharazo
2. Poza Maumivu – Godzilla
9. Bob Manecky (AM Records)
bob
Nyimbo alizotayarisha mwaka huu
1. Nikuite Nani – Jux
2. Hapo Ulipo – Mirror
3. I am Happy – Bob f/ Jux, Ben Pol, Quick Rocka, Young Dee, Gelly wa Rhymes &G-Nako
4. You Wish – M-Rap & Barakah Da Prince
5. Ulimama Nami – Mabeste f/ Barnaba

10. C9 Kanjenje (C9 Records)
11925766_165699530445209_1017268355_n
Nyimbo alizotayarisha mwaka huu
1. Amerudi – Malaika Band
2. Suna – Barnaba
3. Nimpe Nani – Nimpe Nani




Ni hotuba aliyoitoa wakati akilifungua rasmi bunge la kumi na moja ambapo alieleza mipango ya serikali yake na jinsi atavyofanya kazi kwa utofauti, matumizi ya pesa kwenye safari za viongozi nje kwenye awamu iliyopita na mengine.






Wiki chache zilizopita msanii wa Pop kutoka MarekaniRihanna aliweka headlines nyingi sana baada ya kuiweka wazi cover ya Album yake ya nane ANTI inayotegemea kutokaNovember 27 kwenye TIDAL lakini kwenye mitandao mengine  albu hiyo itaanza kupatikana kuanzia tarehe 4 December 2015.


Tarehe 19 November 2015Rihanna aliisogeza #teaser ya Album yake mpya, na kupitia page yake ya Twitter nilikutana na tweet ya Rihanna inayosema, “Ninafuraha ya kushare hiki na nyie!! “, tweet iliyoambatana pia na link itakayokupeleka moja kwa moja kwenye website yake mpya,  ANTIDiaRy.com.



Mpaka sasa Rihanna ameshazisogeza kwetu video tatu kutoka kwenye Album yake mpya, ‘FourFiveSeconds’ (Feat. Kanye West), ‘BBHMM’ na ‘American Oxygen’. Single nyingie zitakazopatikana kwenye Album hiyo ni pamoja na ‘James Joint (Interlude), ‘Higher’, ‘nothing’s Promied, ‘Kiss It Better’, na ‘Only if for a Night’.