August 2016
Alikiba yuko mbioni kuachia silaha yake mpya. Staa huyo wa ‘Aje’ ameonjesha kidogo kile kitakachoonekana kwenye video ya ngoma yake mpya, na mashallah itakuwa na warembo haswaaa.

Staa huyo ameshare picha akiwa mbele ya jumba la kifahari na warembo wanane jijini Johannesburg, Afrika Kusini alikokuwa huko mwezi uliopita.

Kuna msemo mmoja wa kizungu usemao, Great minds think alike, ukiwa na maana ya ‘Akili kubwa hufikiri sawa sawa.

Hii hutokea mara nyingi sana katika sanaa bila ya wasanii husika kulitambua hilo. Unaweza ukakuta wasanii wako sehemu mbili tofauti kwa nyakati tofauti lakini wakatunga mashairi yanayofanana bila kuwepo na wizi wowote.
Kwa mara zote ambapo muingiliano wa idea hutokea na ikiwa tu wameanza wasanii wa nje ya bchi na kisha msanii wa Tanzania akafuata huwa anahukumiwa moja kwa moja kuwa ni mwizi pasipo mashabiki wa Bongofleva kuamini kuwa kuna muingiliano wa wazo kuu(idea).
Lakini je vipi kwa ishu ambazo wasanii wa Tanzania wameanza halafu ndio wakafuata wasanii wa nje? Je nao wamewaiga wasanii wa bongofleva? Ni kweli hatukatai bado hadi leo hii wapo wasanii wa bongofleva wanatafsiri mistari ya wasanii wa nje au kukopi kazi za wasanii wa nje aidha idea za nyimbo, video au uchezaji.
Lakini hapa chini nakuletea mifano ya kazi za wasanii wa bongo na zinazofanana kabisa na kazi za wasanii wa nje lakini wasanii wa Tanzania ndio walikuwa wa kwanza kutoa kazi hizo kabla ya wasanii wa nje na ndio itakayoonesha muingiliano wa idea jinsi ulivyo.
PROFESA JAY (PIGA MAKOFI ) NA BUSTA RHYMES ( MAKE IT CLAP )
Mwaka 2001 msanii wa Hip hop Tanzania Profesa Jay aliamua kuwa msanii binafsi baada ya kukaa kando na kundi lake la ‘Hard Blasters Crew'(HBC) aliloanza nalo muziki mwaka 1994. Na mwaka huo huo alitoa album yake ya kwanza binafsi ‘ MACHOZI JASHO NA DAMU.’
Singo yake ya ‘ Piga Makofi ‘ ilikuwa inapatikana katika albamu hiyo. Mwaka mmoja baadaye,October 13, 2002 msanii wa hiphop kutoka Marekani, Busta Rhymes aliachia wimbo ulioitwa ‘ Make it Clap ‘ aliomshirikisha msanii wa dancehall wa Jamaica, Sean Paul ,ukiwa na maudhui sawa na wimbo wa Professa Jay wa Piga Makofi.
MWANA FA (UNANIJUA UNANISIKIA?) NA LIL WAYNE (JOHN)
Rapa wa zamani wa kundi la East Coast Team(ECT) mara baada ya kumaliza masomo ya shahada ya uzamili ya fedha aliyokuwa akisomea katika chuo kikuu cha Coventry nchini Uingereza, alirudi tena katika ramani ya muziki wa Bongofleva kwa kuachia ngoma iliyojulikana kama ‘ UNANIJUA UNANISIKIA ‘ ambayo ilitoka redioni Feb 23, 2011 na mtandaoni, Feb 25 2011 katika mtandao wa gongamx.com.
Mstari wa tano katika ubeti wa kwanza unasema ‘hela hazilali so ukilala wewe tu.’ Machi 24 mwaka 2011 rapa Lil Wayne aliachia wimbo uliofahamika kama ‘JOHN ‘ ama wengine wakiufahamu kama ‘ IF I DIE TODAY ‘ aliomshirikisha Rick Ross. Mstari wa 15 katika ubeti wa kwanza unasema ‘ The money don’t sleep so Weezy can’t rest ‘ Ukiwa na maana karibia sawa na wa Mwana FA.
Laiti kama wimbo wa Lil Wayne ungekuwa wa kwanza kutoka watu wangedhani kuwa Mwana FA ameuiga mstari huo.
FID Q (NAMBA 8) NA NICK MINAJ (ALL EYES ON YOU)
FID Q : ‘ Anahisi asha niona sehemu tatizo ameshanisahau jina,Unaitwa nani? (FID Q)
Unaishi wapi (Ghetto ) Kazi yako nini? (muziki)
NICK MINAJ: He was like (What’s your name?)
My name Nick (Where you from?) New York in this chick (Choose and pick).
Rapa Fid Q aliichana hiyo mistari katika wimbo alioshirikishwa na Msanii Daz Baba ‘Namba Nane ‘ miaka 10 iliyopita na mistari hiyo ya Nick Minaj inapatikana katika wimbo wa ‘ All eyes on you ‘ alioshirikishwa na rapa aliye kwenye uhusiano naye wa kimapenzi Meek Mill ulioachiwa June 26 2015.
MWANA FA ( AMEEN ) NA DRAKE ( R.I.C.O )
Juni 7 2012 kupitia kipindi cha XXL, Clouds FM. Mwana FA aliachia wimbo ‘AMEEN’ akiwa na Dully Sykes & A.Y ulioandaliwa katika studio ya 4.12, Dully aliyekuwa mtayarishaji wa wimbo huo.
Katika mstari wa tisa wa ubeti wa pili, kuna mstari unasema,”kuna viumbe hata huwajui na bado wana beef na wewe. ” Na huu mstari “How you hate me when I never met the man’ ni wa rapa Drake unaopatikana katika wimbo alioshirikishwa na Meek Mill, ‘R.I.C.O’ uliotoka June 29, 2015.Nadhani umeshapata picha ya ule msemo wa ‘Great Minds think alike. ‘
Imeandaliwa na FARAJI FOWZ ZEGGESON

IG: @xfowz
Twitter: @fowzwheezy
Email : xfowz@icloud.com
Shirikisho la soka duniani (FIFA) janaAgosti 11 limetangaza orodha mpya ya viwango vya kila mwezi kwa timu za mataifa yote duniani huku Argentina ikiendelea kuongoza kwenye chati hizo.
Timu ya Argentina inaendelea kushika namba moja kama timu bora zaidi duniani huku ikiwa na pointi 1585 ikifuatiwa na Ubelgiji (1401), Colombia (1331), Ujerumani (1319) na nafasi ya tano imechukuliwa na Chile yenye pointi 1316.
Kwa upande wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeshuka kwa nafasi moja kutoka 123 mpaka nafasi ya 124 na imefanikiwa kupata pointi 300 ikishika nafasi ya tano kwa nchi za Afrika Mashariki ikiongozwa na Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi.
Aidha viwango hivyo vimeonyesha kuwa kwa Afrika timu ya taifa ya Algeria ndiyo inaongoza ikiwa nafasi ya 32 huku ikiwa na pointi 781 ikifuatiwa na Ghana, Ivory Coast na Senegal ikishika nafasi ya nne
bongo5.com

Video mpya ya muimbaji wa gospel, Angel Benard ‘Ni Wewe.’ Wimbo ulifanywa katika studio za Still Alive jijini Nairobi mtayarishaji akiwa TIM. Video pia imeongozwa na Still Alive. Ni wimbo wenye lengo la kumtambulisha nchini Kenya.

Winga wa kimataifa wa Algeria anayeichezea klabu yaLeicester City kuhusishwa kuondoka King Power msimu huu inawezekana zikawa zimemalizika, Riyad Mahrez anaripotiwa na The Guardian kuwa amekiri kuwa Leicester City hawawezi kumuachia aondoke msimu huu.
 Riyad Mahrez amekubali kubaki Leicester | Picha: Ben Hoskins/Getty

Stori kutoka The Guardian pia zinaeleza kuwa Leicester City wameanza kumsahawishiMahrez aongeze mkataba mpya, licha ya kuwa mkataba wake wa sasa unamalizika 2019 lakini maboss wa Leicester wanaripotiwa kuanza mazungumzo na staa huyo.

Riyad Mahrez has accepted he will not be allowed to leave Leicester this month after talks between his representatives and the Premier League champions’ director of football on Wednesday.

Klabu ya Everton imemsajili rasmi kapteni wa Wales, Ashley Williams kutoka kwa wapinzani wao wa ligi kuu Swansea kwa gharama inayokadiliwa kufikia Euro milioni 12 kwa mkataba wa miaka mitatu.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 31, anakuwa ni mchezaji wa tatu kununuliwa na kocha Ronald Koeman baada ya kiungo wa Senegal Idrissa Gueye na mlinda mlango Maarten Stekelenburg.


Everton have signed Wales captain Ashley Williams from Premier League rivals Swansea for an undisclosed fee, thought to be £12m.
The 31-year-old defender is new manager Ronald Koeman's third summer purchase after Senegal midfielder Idrissa Gueye and goalkeeper Maarten Stekelenburg.
They are also in talks to sign Crystal Palace midfielder Yannick Bolasie and Sunderland defender Lamine Kone.
"I believe the club is going in the right direction," said Williams.
The defender, who has agreed a three-year deal with the Merseyside club, said he was keen to work with former Netherlands international Koeman.
"He's been one of the greatest centre-halves to ever play the game, so I look forward to learning from him," Williams told the club's website.
Swansea had rejected an earlier £10m bid from Everton.
The signing comes a day after England defender John Stones left Goodison Park to join Manchester City for £47.5m.

Katika mitandao ya kijamii Jumatato hii kumezuka mjadala mkubwa baada ya mashabiki wa Diamond Platnumz na AliKiba kuona picha yakutengenezwa inayowaonyesha wawili hao wakipeana mkono.

Wachache kati ya mashabiki hao wanaamini picha hiyo ni yakutengenezwa huku wengi wao wanaamini wawili hao kweli wamepatana.
Pia miongoni mwa mashabiki hao waamini endapo wawili hao watapana basi na muziki wao utashuka kutokana na kupoteza ushindani.
Haya ni baadhi ya maoni ya mashabiki hao kutoka katika mitandao ya kijamii.

Francis Michael

Tukubali kuwa hakuna jambo lisilokuwa na mwisho kwa upendo wao wenyewe wameona tukiendelea hivi mpaka lini tutamaliza tofauti zetu kwa kuwa wasanii hawa wote wanapeperusha bendela yetu ya TZ, Nimefurahi sana kusikia hivi tofauti zao zimekwisha nawaomba kama kweli umekwisha wafanye kolabo yao wasanii hawa wawili watuchezeshe sasa turuke.

Glory Shayo

Haitawezekana kamwe coz Diamond ana wivu na nyimbo za King Kibaa hiyo itabaki tu story.

Joseph Salvatory

Haitatokea kumaliza tofauti zao hadi Diamond arudishe ile kolabo aliyo mshilikisha Kiba na Kiba kumfunika Diamond, kwa roho mbaya ya Diamond akaifuta.

Veronica Godluck

Elewa kwamba kuna maisha mengine baada ya muziki, na uwezi jua mungu amepanga nini juu yako, so haina haja ya mabifu chamsingi kila mtu awangalie mashabiki wake wanataka nini. Kumake money ndio kila kitu.

Albert Kariuki Tz

Binafsi nita jihisi vibaya kwa kuwa ule ushindani hautakuwepo na muziki yao ni kama vile ita chuja.
Juma Masifia 
Umesema ukweli wote coz kama hawa mastari wangekuwa wana bifu lazima serikali au baraza lao lingeingilia kati na kupelekana mahakamani siyo daily tunasikia mambo tofauti mengi kwenye media na midomo ya watu kumbe hakuna chochote isipokuwa ushabiki wa watu na media
Haruna Hamisi 
Kama wakiungana muziki nao utakuwa umekwisha kwa Diamond & Ally Kiba kwakuwa sasa hivi upinzani wa wasanii hao tu ni gumzo unafanya kuwapa mafanikio makubwa sana kiukweli sasa hivi muziki wa bongo fleva, kwenye soko wameliteka Diamond & Ali Kiba, yaani tunawaangalia wao tu Kiba katoa nini na Mond katoa nn? Sasa wakiungana muziki kwao hakuna tena, kwa hiyo bifu linachangia muziki kwenda mbali.