Kuna msemo mmoja wa kizungu usemao, Great minds think alike, ukiwa na maana ya ‘Akili kubwa hufikiri sawa sawa.

Hii hutokea mara nyingi sana katika sanaa bila ya wasanii husika kulitambua hilo. Unaweza ukakuta wasanii wako sehemu mbili tofauti kwa nyakati tofauti lakini wakatunga mashairi yanayofanana bila kuwepo na wizi wowote.
Kwa mara zote ambapo muingiliano wa idea hutokea na ikiwa tu wameanza wasanii wa nje ya bchi na kisha msanii wa Tanzania akafuata huwa anahukumiwa moja kwa moja kuwa ni mwizi pasipo mashabiki wa Bongofleva kuamini kuwa kuna muingiliano wa wazo kuu(idea).
Lakini je vipi kwa ishu ambazo wasanii wa Tanzania wameanza halafu ndio wakafuata wasanii wa nje? Je nao wamewaiga wasanii wa bongofleva? Ni kweli hatukatai bado hadi leo hii wapo wasanii wa bongofleva wanatafsiri mistari ya wasanii wa nje au kukopi kazi za wasanii wa nje aidha idea za nyimbo, video au uchezaji.
Lakini hapa chini nakuletea mifano ya kazi za wasanii wa bongo na zinazofanana kabisa na kazi za wasanii wa nje lakini wasanii wa Tanzania ndio walikuwa wa kwanza kutoa kazi hizo kabla ya wasanii wa nje na ndio itakayoonesha muingiliano wa idea jinsi ulivyo.
PROFESA JAY (PIGA MAKOFI ) NA BUSTA RHYMES ( MAKE IT CLAP )
Mwaka 2001 msanii wa Hip hop Tanzania Profesa Jay aliamua kuwa msanii binafsi baada ya kukaa kando na kundi lake la ‘Hard Blasters Crew'(HBC) aliloanza nalo muziki mwaka 1994. Na mwaka huo huo alitoa album yake ya kwanza binafsi ‘ MACHOZI JASHO NA DAMU.’
Singo yake ya ‘ Piga Makofi ‘ ilikuwa inapatikana katika albamu hiyo. Mwaka mmoja baadaye,October 13, 2002 msanii wa hiphop kutoka Marekani, Busta Rhymes aliachia wimbo ulioitwa ‘ Make it Clap ‘ aliomshirikisha msanii wa dancehall wa Jamaica, Sean Paul ,ukiwa na maudhui sawa na wimbo wa Professa Jay wa Piga Makofi.
MWANA FA (UNANIJUA UNANISIKIA?) NA LIL WAYNE (JOHN)
Rapa wa zamani wa kundi la East Coast Team(ECT) mara baada ya kumaliza masomo ya shahada ya uzamili ya fedha aliyokuwa akisomea katika chuo kikuu cha Coventry nchini Uingereza, alirudi tena katika ramani ya muziki wa Bongofleva kwa kuachia ngoma iliyojulikana kama ‘ UNANIJUA UNANISIKIA ‘ ambayo ilitoka redioni Feb 23, 2011 na mtandaoni, Feb 25 2011 katika mtandao wa gongamx.com.
Mstari wa tano katika ubeti wa kwanza unasema ‘hela hazilali so ukilala wewe tu.’ Machi 24 mwaka 2011 rapa Lil Wayne aliachia wimbo uliofahamika kama ‘JOHN ‘ ama wengine wakiufahamu kama ‘ IF I DIE TODAY ‘ aliomshirikisha Rick Ross. Mstari wa 15 katika ubeti wa kwanza unasema ‘ The money don’t sleep so Weezy can’t rest ‘ Ukiwa na maana karibia sawa na wa Mwana FA.
Laiti kama wimbo wa Lil Wayne ungekuwa wa kwanza kutoka watu wangedhani kuwa Mwana FA ameuiga mstari huo.
FID Q (NAMBA 8) NA NICK MINAJ (ALL EYES ON YOU)
FID Q : ‘ Anahisi asha niona sehemu tatizo ameshanisahau jina,Unaitwa nani? (FID Q)
Unaishi wapi (Ghetto ) Kazi yako nini? (muziki)
NICK MINAJ: He was like (What’s your name?)
My name Nick (Where you from?) New York in this chick (Choose and pick).
Rapa Fid Q aliichana hiyo mistari katika wimbo alioshirikishwa na Msanii Daz Baba ‘Namba Nane ‘ miaka 10 iliyopita na mistari hiyo ya Nick Minaj inapatikana katika wimbo wa ‘ All eyes on you ‘ alioshirikishwa na rapa aliye kwenye uhusiano naye wa kimapenzi Meek Mill ulioachiwa June 26 2015.
MWANA FA ( AMEEN ) NA DRAKE ( R.I.C.O )
Juni 7 2012 kupitia kipindi cha XXL, Clouds FM. Mwana FA aliachia wimbo ‘AMEEN’ akiwa na Dully Sykes & A.Y ulioandaliwa katika studio ya 4.12, Dully aliyekuwa mtayarishaji wa wimbo huo.
Katika mstari wa tisa wa ubeti wa pili, kuna mstari unasema,”kuna viumbe hata huwajui na bado wana beef na wewe. ” Na huu mstari “How you hate me when I never met the man’ ni wa rapa Drake unaopatikana katika wimbo alioshirikishwa na Meek Mill, ‘R.I.C.O’ uliotoka June 29, 2015.Nadhani umeshapata picha ya ule msemo wa ‘Great Minds think alike. ‘
Imeandaliwa na FARAJI FOWZ ZEGGESON

IG: @xfowz
Twitter: @fowzwheezy
Email : xfowz@icloud.com
Share To:

Red Chapter

Post A Comment:

0 comments so far,add yours