Kundi maarufu la Uingereza la One Direction,
huingiza pauni 19,000 kila siku ambazo ni zaidi ya
shilingi milioni 62.

Waimbaji hao waliopata mafanikio baada ya kuwa
chini ya usimamizi wa Simon Cowell kupitia kipindi
cha The X Factor mwaka 2010, huingiza kiasi hicho
cha fedha kufuatia taarifa zao za fedha
 zilizochapishwa na Companies House.

One Direction walitengeneza faida ya jumla ya
 £35m na kampuni yao 1D Media mwaka jana
ingawa mwenzao Zayn Malik alijiondoa na
kuwaacha Harry Styles, Liam Payne, Niall Horan na
Louis Tomlinson.

Pamoja na mafanikio hayo, vijana hao wameamua
kupumzika mwakani baada ya kuachia album tano
na kufanya ziara nne.
Share To:

Red Chapter

Post A Comment:

0 comments so far,add yours